Habari Kali
Loading...

AUNT,WEMA MAJANGA MATUPU......

Baada ya kula viapo vya kutozikana, wasanii wawili wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Aunt Ezekiel Grayson wamejikuta wakiangua vilio wakati wakipatanishwa na rafiki yao mkubwa ambaye ni pedeshee anayejulikana kwa jina la Daudi Mambya.
Aunt Ezekiel akimbembeleza Wema baada ya kupatanishwa.
Habari kutoka kwa shuhuda wetu zilieleza kwamba, tukio hilo lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Ufukwe wa Coco jijini Dar ambapo Daudi aliwaita kwa mwaliko wa mishikaki bila wenyewe kujua kinachoendelea.
Habari zilieleza kuwa, Daudi ambaye kwake huwa hawafurukuti, amekuwa akiumizwa mno na tofauti ya wasanii hao kwa sababu ni watu walikuwa wakipendana hivyo kugombana kwao kulikuwa kunaleta shida kwa marafiki zao wengine.
Imefahamika kwamba, Daudi alitumia ujanja wa kuzungumza na kila mmoja kwa wakati wake ambapo alibaini kuwa hakuna aliyekuwa tayari kupatana na mwenzake.
Ilisemekana kuwa, Daudi alitumia ujanja wa kitaalamu ili kila mmoja kumuweka sawa bila kujijua.
“Unajua Daudi ni rafiki yao sana, sasa hakuwa anapendezwa na tatizo ambalo limejitokeza hivyo alitumia njia tofauti ili kuweza kuwakutanisha pamoja tena waweze kupatana,” alieleza mtoa habari huyo.
Wakiwa na rafiki yao Daudi Mambya anayedaiwa kuwapatanishwa.
Ilielezwa kwamba Daudi alianza kwa kumtafuta Wema na kumpeleka Coco Beach akimuambia kuwa anataka akamnunulie mishikaki huku wakati huohuo akimwambia Aunt naye wakutane ufukweni hapo.Shushushu wetu alizidi kufunguka kuwa Daudi alitangulia Coco na Wema, huku akifanya mawasiliano na Aunt na baada ya muda, Aunt naye aliwasili huku kila mmoja akibaki katika mshangao usioelezeka baada ya kukutana uso kwa uso.
Sosi huyo alisema kuwa Wema na Aunt walipoonana kila mmoja alikuwa kimya lakini Daudi aliamua kuwasomea risala ndefu iliyomwingia kila mmoja.Mambo yakipokaa vizuri, wawili hao walishuhudiwa wakiwa wamekumbatiana huku kila mmoja akiangua kilio kilichochukua takribani nusu saa hivyo kufanya eneo hilo kuwa kama kuna msiba.
“Yaani mpaka Daudi mwenyewe alidondosha machozi baada ya Wema na Aunt kukumbatiana na kuanza kulia.
“Yaani ilikuwa simanzi kubwa sana,” alimalizia shuhuda huyo.Akizungumza na gazeti hili, Daudi alisema kuwa aliamua kuwapatanisha wawili hao kwa kuwa alikuwa hapendezwi na tatizo hilo na kwamba wote ni rafiki zake.
Kwa upande wake, Aunt alifunguka ya moyoni:
“Tulipokutana kila mtu alijua tatizo lake na tukaona ni mambo ya kijinga, ikabidi tuweke tofauti pembeni maisha yaendelee.”
Wema alisema: “Mambo ya kugombanagombana hayana msingi na kwa vile ni mtu mzima (Daudi) aliwakutanisha, nikaona yaishe.”Wema na Aunt ambao walikuwa marafiki wakubwa waliingia kwenye mgogoro hivi karibuni baada ya Wema kumtuhumu Aunt kuunga mkono shoo ya Zari All White Party ya mwanadada Zari Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye ni mpenzi wa aliyekuwa mpenzi wa Wema, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz

Mmmh! Hivi Wema alimkosea nini Diamond??? Mbona “kamtaja” tena kwenye wimbo wake mpya???


Mmmh! Hivi Wema alimkosea nini Diamond??? Mbona “kamtaja” tena kwenye wimbo wake mpya???
     
    Leo video ya muziki ya Msanii Diamond platnumz ya wimbo wa My Number one imetoka rasmi kwenye Television na mitandao mbalimbali ya kijamii na kusema ukweli ni moja ya video nzuri sana za muziki hapa nchini na sio siri kijana huyu wa bongofleva amefanya kazi kubwa sana na anastahili pongezi.
    Baada ya kuisikiliza kwa makini nyimbo hii yenye mahadhi flani ya kiafrika zaidi tulifika kwenye dakika ya 2 na sekunde 50 (2:50) ya nyimbo hii na ndipo ukatokea “ubishi” ambao tukaona sio mbaya tukiupeleka kwa wasomaji wetu ili kupata maoni Zaidi.
    Katika sehemu hii ya mwisho ya nyimbo hii Diamond anatamka maneno ambayo baadhi ya watu tuliokuwepo katika mabishano hayo tunasema kuwa yanamlenga mwanadada wetu muigizaji, Wema sepetu kama “vijembe” kwakwe, diamond anamalizia wimbo wake kwa kusema “TUACHE TULALE” maneno amabyo kwa wale wanafuatilia habari za watu hawa wawili yalioongewa na mpenzi wa diamond wa sasa VJ penny kwenye tukio la wapenzi hao kumrekodi mwanadada Wema Sepetu kwenye simu alipokuwa akimbembeleza mpenzi wake wa zamani (Diamond Platnumz) warudiane, tukio liliotokea miezi kadhaa iliyopita.
    Swali likawa, Je maneno haya yatakuwa yanamlenga Wema??? Kama siyo kwanini Diamond ayatamke sehemu ambayo hata haihusiani nayo kwenye wimbo???

    MMH, MAKUBWA: , IRENE UWOYA,WEMA SEPETU, JB, MZEE MAJUTO NA JACKLINE WOLPER WAMTETEA MANAIKI SANGA KUHUSU PICHA ZA UCHI....!












    Wasanii mbalimbali wanaunda kundi la Bongo Movie nchini ambao wameshiriki kwenye filamu ya msanii Manaiki Sanga iitwayo Wake Up wamemtetea msanii mwenzao kuhusu kashfa ya picha za uchi alizowahi kupiga miaka ya nyuma. Wakiongea na gazeti hili hivi karibuni wakati wakiigiza filamu hiyo iliyowashirikisha zaidi ya wasanii 36 walisema kuwa binadamu wote wanatakiwa kusahau madhambi ya mtu kwa vile yalishapita ni vyema watu wakaangalia ya sasa na yajayo. Wasanii hao ambao ambao kila mmoja aliongea jinsi anavyoona lakini kila mmoja alionekana kumtetea Manaiki kwa tukio alilowahi kulifanya. Mmoja wasanii hao ambae nae ni mshiriki ni Jackline Wolper baada ya kuulizwa na mwandishi wetu anazungumzia matukio ya ukatili ya msanii huyo kwa wanawake aliyowahi kuafanya ambapo alijisema “ Kiukweli Manaiki aliwahi kuteleza kama ambavyo angeweza kuteleza binadamu mwingine au mimi na wewe hivyo ni vyema tuka sahau hayo tusiendelee kumuhukumu Manaiki kwa madhambi yaliyopita si vizuri” Alisema Wolper Aidha nae Irene Uwoya ambae aliwahi kutuhumiwa kutembea na Manaiki yeye alisema hivi “ Ndugu yangu mimi upande wangu naweza kusema kuwa jamii inapaswa kumsamehe Manaiki sisi sote ni binadamu na tunakosea ni vyema tukasahau yaliyopita tayari picha ziko mitandaoni na kama anavyoeleza mwenyewe alipoteza Computer yake na kulikuwa na picha zake za sili” Alisema Uwoya Mzee Majuto ambae ni swahiba mkubwa wa Manaiki alisema “Mwanangu binadamu hatujakamilika Manaiki si kijana mbaya ndiyo maaa unaona wasanii wote hawa tunampa sapoti amekuwa na ushirikiana na wenzake sana, kuhusu hizo picha ni jambo la kusahau kwa vile lilishapita tugange yajayo watanzania subirini kuipokea filamu yake mpya inaitwayo Wake Up ambayo ni kama zawadi kwa watanzania” Alisema msanii huyo mkongwe Kajala Masanja ambae kwa sasa wameingia mkataba na Manaiki kwa ajili ya kufanya kazi pamoja yeye upande wake alisema “ Ni kweli kati ya watu walioumia sana kuona zile picha ni mimi Manaiki ni kama mdogo wangu ndiyo maana nimeamua kumchukua na kuwa nae pamoja na kumuweka sawa kisaikolojia kwa vile tayari zile picha zilikuwa zimemuathiri “ Alisema Kajala Wasanii karibia wote walioshiriki filamu hiyo yaExpendables ya Tanzania iitwayo Wake Up iliwashirikisha wasanii zaidi ya thelathini na sita huku iliongozwa na Lamata na kushutiwa na kampuni ya Manaiki Production iliyopo Itumbi Hotel. Wasanii walioshiriki filamu hiyo ya Wake Up ni Irene Uwoya, Jackline Wolper, Gabo, Othuman Amri “King Majuto” Kajala, Yusuph Mlela, Tausi, Aisha Boko, Hemed Suleiman, Quickrocker, Kupa,Duma, Mama Abdul, Flora Mvungi, Tracy Moshi, Hemed Kavu “HK” kwa upande wa wanaumziki ni Country Boy, Nas B, Kiss, Juta B, akiwemo mwenyewe Manaiki Sanga ambae ndiye staa wa filamu hiyo na wengine wengi

    Wema Sepetu azua gumzo kwenye mtandao baada ya kumuita Diamond "kaka"

    Wema Sepetu azua gumzo kwenye mtandao baada ya kumuita Diamond

     
    Huku macho na masikio ya wananchi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania yakiwa kwenye bunge la katiba linalojadili lile sakata la tegeta ESCROW, mwanadada Wema sepetu ameamua naye kuzua gumzo kwenye mtandao baada ya kutoa salamu ya pongezi kwa kijana Naseeb al maarufu kama Chibu dangote ama Diamond platnumz kwa ushindi wake wa tuzo 3 kwenye tuzo za Channel O MUSIC AWARDS zilizofanyika huko Afrika ya kusini akitumia neno KAKA katika sentensi yake kitu ambacho kimezua minong’ono ya hapa na pale kwenye mtandao ule maarufu wa kijamii wa picha nchini.
    Katika post yake hiyo Wema aliandika
     “…Hongera tele ziende kwa kaka platnumz... I must say he did Tanzania proud..”   na kufanya watu waanze kufunguka ya kwaio ya moyoni kuhusu kauli hiyo na baadhi yao walisema haya.

    MELA : “Leo kawa kaka!!!!!! Aiseeee mapenz ya mastaa mafupi kama mkia wa kondoo”

    “ LILY: “et kaka plutnums heheheheh wema bwana”

    “PIERE: mara hii kaka tena?? Ohhhhhh”

    ANNA: “hao ni wakuwaacha kesho.tu.watakua tena pamoja”
    Katika tuzo hizo, diamond alisindikiwa na anayesemekana kuwa kipenzi chake cha sasa, mwanadada Zari ktukoa nchini Uganda, pamoja na mama yake mzazi na team ya wasafi.

    Nini maoni yako mdau kuhusu ishu hii? 

    WEMA NA DIAMOND WAKIPONA SAFARI HII HAKIKA WAKACHINJE KUKU MWEKUNDU, SERIKALI YAWAKALIA KOONI ANGALIA HAPA ..!


    IMEBAINIKA kuwa wapo baadhi ya wasanii wa filamu na muziki nchini kuwa na tabia ya kujipiga picha za uchi na kuzitumia visivyo ikiwemo kuzituma kwenyemitandao hali inayochangia mmomonyoko wa maadili nchini.
    CHEKI PICHA CHAFU HAPO CHINI
    Sakata la kusambaa kwa picha hizo zisizokuwa na maadili mitandaoni zikiwemo za watu maarufu hapa nchini leo limeibuka tena bungeni likiwa na sura mpya huku baadhiya wabunge wakitaka kujua serikali inachukua hatua gani juu ya picha zilizosambaa juzi zinazomuonesha mmoja wa wabunge (jina kapuni) akiwa na binti mdogo ambazo mwenyewe alikanusha na kudai si za kwake.
    Moto huo ulizidi kuwaka bungeni leo katika kipindi cha maswali na majibu ambapo Mbunge wa Mchinga (CCM), Mhe. Said Mtanda amehioji serikali wamechukua hatua 

    gani dhidi ya vitendo vya uchapaji wa picha zisizozingatia maadili huku akiwataja Wema na Diamond kupiga picha wakiwa chumbani na kuweka kwenye mitandao.
    Katika majibu yake Naibu waziri Habari Utamaduni na Michezo Mheshimu Mkamia, alijibu kuwa serikali imebaini juu ya matumizi hayo ya picha
    Mheshimiwa Habib Mnyaa aliuliza swali la nyongea kwa wizara ya mawasiliano ya sayansi na teknolojia ambapo jibu hilo lilijibiwa na waziri wa mawasiliano
    Katika majibu yake waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia Prof. Makame Mbarawa anasema “Mhe. Spika kuhusu picha zisizokuwa na maadili zinazowekwa katika mitandao na watu maarufu na hata wasiokuwa maarufu serikali imeanza kuandaa kanuni zitakazokuwa zikifuatilia Online Content ambapo itaanza kuchukua hatua baada ya kufuatilia juu ya picha hizo na kuchukua hatua madhubuti”.
    Baada ya kauli hiyo Spika wa bunge Mhe. Anne Makinda alikazia akitaka majibu juu ya picha za juzi zilizosambaa zikimuonyesha Mhe. Komba akiwa na binti mdogo ambazo mwenyewe alisema si zake na wabunge kuonekana wakitaka majibu ambapo Mhe. Mbarawa anasema.
    “Mhe. Spika kuhusu picha za juzi zilizosambaa mitandaoni tunazifuatilia kujua zimeanzia wapi na taarifa zake zikoje kwani hata mimi bado sijaziona ila tutachukua hatua tutakapobaini zilipotoka.

    MAKALIO YA WEMA SEPETU NI NOUMA YAMDATISHA MC WA MTV MAMA HADI KUFIKIA HATUA YA ******SOMA HAPA KWA HABARI KAMILI

    HII NDIO SENTENSI ALIYOITOA MC WA MTV MAMA INAYOHUSU MAKALIO YA WEMA SEPETU

    Kama ilivyo kwa tuzo zozote maarufu duniani, mara nyingi ma’MC wa show hizo huwa wanapenda kumwaga maneno mengi sana ya utani, ila hii ni kali zaidi, bila kujijua mwenyewe wakati akiwa anaendelea kutangaza, alitokea kuwaponda watu maarufu duniani, akiwemo Kim Kardashian ambaye anajulikana kama ni mwanamke mwenye umbo zuri zaidi, “I’ve seen beautiful women here with butts that make kimkardashian‘s look like Miley Cyrus.(“nimekuja hapa nimeona wanawake wenye maumbo mazuri, yanavyomfanya Kim Kardashian aonekane kama Myle Cyrus”) – alitamka wazi wazi MC wa tuzo hizo za MTV MAMA.

    Watu wenye maumbo kama Wema Sepetu na wanawake wengi wa huko nchini South Africa achilia mbali wageni waaalikwa kutoka nchi mbali mbali za africa, kwa jinsi walivyo umbika kwa asili ya maumbo yao ya ki-africa, yalimfanya hadi MC ambaye ndiye mchekeshaji muigizaji maarufu huko hollywood maarufu kama Marlon Wayans, ashundwe kujizuia na kutamka maneno kama hayo hadharani.

    DIAMOND AFUNGUKA KUHUSIANA NA KUKOSA TUZO ZA MTV MAMA HUKO SOUTH...BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI>>>>>>>>

    HOT NEWS: KWA MARA YA KWANZA BAADA YA KUKOSA TUZO ZA MTV...!



    Macho na masikio ya Watanzania wengi kwa siku ya Jumamosi June 07 yote yalielekezwa Durban Afrika Kusini sehemu ambako zilikua zikitolewa tuzo za wateule wa MTV Afrika 
    Music Award ‘MAMA’.
    Furaha tuliyokuwa nayo Watanzania ilikua kubwa baada ya kuona kijana kutoka nyumbani Tanzania kuwa ni miongoni mwa vijana wanaochuana kwenye tuzo hizo tena akiwa vipengele viwili,ingawa bahati haikua njema kwa Diamond kwani hakufanikiwa kupata.


     Baada ya kutangazwa washindi hao na yeye kutokuwepo Dimaond Platnumz ameandika maneno haya kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii>’Maisha ni Hatua.. Nafkiri kwa mwaka huu ile ndio ilikuwa hatua yetu kwa MTV…Cha muhimu ni kujua wapi tulipokua mwaka jana na wapi tulipo leo… pia kujifunza na kujua ni nini cha kuongeza zaidi ili Next

    HAKIKA WEMA SEPETU NAE ANASTAHIRI KUPEWA TUZO, ANGALIA LIST YA WANAUME ALIOKULA NAO URODA

     Wema Sepetu ni miongoni mwa wasanii wenye mvuto sana hapa Tanzania na tunaweza kusema hata Afrika Mashariki. Amejipatia umaarufu mara ya kwanza baada ya kushinda taji la Miss Tanzania mwaka 2006. Baada ya hapo alianza kumake headlines kwa skendo za mapenzi kabla hajaingia rasmi kwenye tasnia ya filamu, na aliyemuingiza alikuwa ni Marehemu Steven Kanumba. Kwa kipindi hiki kisichozidi miaka 10 ya umaarufu wake amefanukiwa kufanya mambo makubwa katika tasnia ya filamu kwani ameonesha kipaji cha hali ya juu sana. Licha ya hayo umaarufu wake unakuzwa zaidi na skendo za hapa na pale na mara nyingi ni skendo za mapenzi. Leo tumeamua kuwaletea list ya wanaume aliotoka nao mpaka sasa kwa kipindi hiki cha miaka 8 ya umaarufu wake.
    1. MR. BLUE
    Mara baada ya kuwa Miss Tanzania mwaka 2006 Wema kama kawaida yake hakutaka kuwa na uhusiano na mtu asiyekuwa na jina mjini. Aliamua kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na mwanamziki huyu ambaye kwa kipindi hicho alikuwa ndio anatawala soko la mziki wa kizazi kipya. Hatujui waliachana vipi lakini hivi karibuni Mr. Blue alinukuliwa akisema kuwa Wema alimfilisi kipindi anatoka nae. Kama hukusoma hii habari ISOME HAPA 

    2. T.I. D
    Baada tu ya kuachana na Mr. Blue tulisikia tetesi kuwa anatoka na Msanii mwingine Khalid Mohamed almaarufu kama TID. Hatukujua mwisho wa uhusiano wao ulikuwaje lakini baada ya kuachana tulisikia TID ametoa wimbo ambao ulikuwa ni kama dongo kwa Wema, ulikuwa unaitwa NILIKATAA

    3. STEVEN KANUMBA
    Baada ya kuruka ruka huku na kule hatimaye Wema aliangukia kwa Aliyekuwa nguli wa tasnia ya filamu hapa Bongo Marehemu Steven Kanumba (RIP BROTHER). Mahusiano yao yalimake headline mjini lakini yaliisha vibaye kwani kila Mtanzania alijua baada ya Wema kuwekwa selo na Kanumba baada ya kumfanyia fujo. Japokuwa waliachana lakini Wema humshukuru Kanumba kila siku kwani ndiye aliyemuingiza katika tasnia ya filamu baada ya kugundua kuwa ana kipaji sana.

    4. JUMBE
    Huyu dogo dogo kwa kweli hakuwa maarufu lakini alikuwa na pesa, nahisi hicho ndicho kitu kilichomfanya Wema ahamiashie majeshi yake baada ya kutoka kwa KANUMBA

    5. CHALZ BABA
    Baada ya kutoka kwa Jumbe, Wema alihamishia majeshi kwa Mwanamuziki wa dansi Chalz Baba enzi hizo akiimbia bendi ya African Stars.

    6. DIAMOND
    Kutoka kwa Chalz BABA, Wema alihamishia mapenzi yake kwa mwanamuziki Diamond Platnumz. Kama kawaida yake alitazama ni nani anayeng'ara kwenye tasnia ya burudani bongo na akafankiwa kumtia himayani Diamond Platnumz enzi hizo Diamond ndio alikuwa msanii anayeng'ara zaidi baaada ya kutwaa tuzo tatu katika TUZO ZA KILI MUSIC AWARD. Mahusiano yao yalikuwa hot kiasi kwamba yaliweza kuzua gumzo katika mitandao ya kijamii kabla ya kuachana.

    7. CLEMENT
    Huyu jamaa alimnasa Wema mara tu baaada ya kuachana na Diamond, alitumia pesa alizokuwa nazo na Wema alianza kuonyesha jeuri ya pesa alizokuwa anapewa na CK. Alinunua nyumba ya Mil 400, akafungua Ofisi yenye thaman ya mil 85 na kubadilisha magari kama nguo. Mwisho wa mapenzi ya Wema na CK ulikuwa mbaya kwani Wema alipokonywa vitu vyake alivyokuwa amepewa na kuishiwa jeuri tena mjini.

    8. DIAMOND TENA
    Baada ya kuachana na CK aliamua kurudisha majeshi kwa Diamond ambapo mpaka sasa wako wote na wamekuwa wakimake headline kwenye social media kila siku. teenz Choice tunawatakia kila la kheri ili tunamuomba Wema atulie tu kama kweli hapo amependa aweke mizizi. Kila la KHERI


    JIONEE PICHA ZA AFTER PARTY YA DIAMOND BAADA YA KUNYAKUA TUZO 7 ZA KTMA


    CHUKUA DAKIKA 3 TU KUSIKILIZA WEMA ALICHOKISEMA KUHUSU KUPORWA MCHUMBA WAKE NA RAFIKI YAKE KIPENZI NAIMA


    Kwa mujibu wa chanzo kinachodaiwa kuongea na gazeti hilo la udaku la kampuni ya Global Publishers, Clement ameamua kutembea na Naima ili kumuumiza roho Wema. “Unaambiwa nyuma ya pazia stori ni kwamba anataka Wema aumie ndiyo maana ameamua kubanjuka na Naima huku akijua kabisa kuwa ni marafiki,” gazeti hilo limekinukuu chanzo hicho.
    Tayari kuna picha ya Naima inayomuonesha akiwa amejichora tattoo yenye jina la Clement.
                                                          



    msikilize wema hapa alichoisema Wema hapa chini

    18++AIBU~~PICHA ZA UTUPU ZA YULE DEMU ALIYE MPIKU WEMA SEPETU KUDATE NA YULE KIGOGO ZA VUJA, TAZAMA HAPA;

     Rafiki kipenzi wa Wema Sepetu mwanadada Naima ambaye ndiyo anamiliki mpenzi wa zamani wa shosti yake anayejulikana kwa jina la Clement ambaye ni kigogo na pedeshee wa mjin hapa, hivi karibuni aliachia picha mtandaoni akiwa mtupu na kufanya watu washikwe na mshangao na kumshangaa dada huyu.
    https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg5h5ENbCHPzBNULWh46bsSncr1ebIVlorF7gl_keoEnZtP2Yj_dyBAlmVetHvqSvwqmauqdXk12Qz3Yebc_pagUWPcfvoR8MJ_xEErMxakYxoiCEFuCShUftcFF9bgaGZ5Kp1N6ENHXrc/s1600/Screenshot_2014-02-02-17-05-35.jpg 
    CREDIT-SWAHILI TZ

    WEMA NAE AJITABIRIA KIFO ..."NIKIFA NIAGWE UWANJA WA TAIFA"


    Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ambaye huwa haishiwi habari, ameibuka na jipya akidai kuwa akifa leo au kesho basi aagwe Uwanja wa Taifa jijini Dar, Ijumaa Wikienda limemtegea sikio.
    Wema Isaac Sepetu.
    Miss Tanzania huyo wa 2006/07 ambaye anakimbiza kwenye sinema za Kibongo alifunguka hayo wikiendi iliyopita wakati akiwa safarini kuelekea jijini Arusha ambapo msanii anayemilikiwa na kampuni ya Wema ya Endless Fame Production aliyetajwa kwa jina moja la Mirrow alikwenda kuangusha shoo pande hizo.
    Wema aliyasema hayo alipokuwa akichangia mada ya utabiri wa mtoto wa aliyekuwa mtabiri bingwa, marehemu Sheikh Yahya Hussein, Maalim Hassan Hussein aliyetabiri kwamba wasanii wengi wenye majina makubwa watakufa mwaka 2014.
    Mwanadada huyo alisema mastaa wengi wameaga dunia na kuagwa kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni lakini yeye itakuwa Uwanja wa Taifa.
    Alitolea mifano ya waliokuwa mastaa kama Steven Kanumba, Albert Mangweha ‘Ngwea’, Julius Nyaisangah ‘Anko J’ na wengine kuwa waliagwa Leaders lakini kwa namna ambavyo jina lake ni kubwa ndani na nje ya Bongo viwanja hivyo havitatosha.
    “Mimi nakwambia kabisa, pale Leaders hapatatosha. Kama nikifa leo au kesho, niagwe Uwanja wa Taifa ili kila mtu apate nafasi. Naamini watu watakuwa wengi sana so Leaders hapatatosha,” alisema staa huyo mkubwa anayeminya kilamalavidavi na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
    Ijumaa Wikienda lilipododosa kwa marafiki zake wa karibu lilitonywa kwamba tayari jambo hilo alishawaeleza na kwamba aliomba iwe hivyo.
    Mbali na wasanii, Maalim Hassan alitabiri pia kuwa mwaka huu kuna mwanasiasa mkubwa atakufa na utakuwa msiba wa kitaifa, vifo vya wanahabari na malumbano makubwa juu ya serikali tatu.
    Wiki iliyopita ilijaa simanzi baada ya kufariki dunia kwa watu maarufu kama mchekeshaji wa Futuhi ya Star TV, Omary Majuto ‘Mzee Dude’, mpiga ngoma wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Soud Mohamed ‘MCD’, mwigizaji wa Bongo Movies, Victor Peter na mtangazaji wa East Africa Radio, Kenneth Kidago Lyanga

    HIVI NDIVYO JOKATE ALIVYOMSHANGAZA WEMA STEGINI KWA KUMWAGIA MINOTI ....MATUKIO KATIKA PICHA ...!!

    IMG-20140202-WA0012

    Unaweza kujikuta ukishindwa kuielewa hii hali lakini inabidi ukubaliane na ukweli halisi wa hiki kilichotokea,Jokate na Wema historia yao ilianzia kwenye shindano la kumtafuta Miss Tanzania 2006 ambapo Mshindi alikua ni Wema Sepetu akifatiwa na Jokate kisha mshindi wa tatu akiwa Lissa Jensen.

    2006

    Headline zilikuja kutengenezwa tena zikiwahusisha warembo hawa kuonekana wako na mtu mmoja ambapo magazeti mengi yaliandika mahusiano haya  yaliyokua yakimhusu Diamond Platnumz kutoka na warembo hawa.

    IMG-20140202-WA0009

    Kimepita kimya kirefu sana juu ya hawa watu wawili hadi usiku wa February 01 huko Arusha kwenye Tamasha la Divaz Night Endless Fame ambalo ndani yake kulikua na mastar kadhaa akiwemo Wema Sepetu,Aunt Ezekiel,Martin Kadinda,Kajala,Zamaradi Mketema,Chid Benzi,Mirror,Jordan na wengine kibao.

    IMG-20140202-WA0011
    Wakati Madam Wema Sepetu akimwaga mauno kwenye jukwaa bila kutegemewa na mtu yoyote Jokate alipanda Jukwaani na kuanza kumtunza Wema pesa na wakati huo Wema alikua akicheza Wimbo wa Diamond My Number One ‘Ngololo’ ambapo Jokate aliungana na Wema kuucheza Wimbo huo.

    IMG-20140202-WA0008


    BOFYA HAPA KUITAZAMA VIDEO: WEMA SEPETU KATIKA BEHIND SCENE YA JARIDA LA VIBE...MMHHH NI HATARI SANA...!!

    CHEKI VIDEO HAPA CHINI..

    WEMA SEPETU AJIKOSHA KILA AGUSACHO NI DIAMOND ??.........

    VibeTZ-magazine-Issue-3

    Wema Isaac Sepetu akiwa kwenye cover ya Vibe Magazine Tz
    Ndani amezungumzia vita vingi yakiwemo mahusiano yake na Diamond Platnumz.
    Katika mahojiano na gazeti hilo maarufu Wema amemtaja Diamond kuwa ndio mwanaume wa maisha yake
    “Yes definitely he’s the greatest love of my life. Naseeb ndio mwanaume wa maisha yangu and maybe that’s the only reason why nipo karibu naye sana.”

    Alipoulizwa if they are dating Wema alisema
    “Hahahahahah……no comment hehehe.’


    Wema pia amezungumzia maisha yake kwa ujumla kuhusu kazi zake, kampuni yake na namna anavyotumia umaarufu wake na mamb mengine mengi .Pata nakala yako


    WEMA ,DIAMOND WAFUNGIWA KAZI SOMA KILICHOJIRI..

    Waandishi Wetu
    HABARI mpya! Mama wa Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu, Mariam Sepetu anadaiwa kuingia rasmi mitaani akiwasaka wapenzi, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Wema, chanzo cha uhakika kimesema na Amani.
    Wema na Diamond wakiwa katika pozi la kimahaba.
    Kwa mujibu wa chanzo hicho makini, mama Wema ameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kusikia taarifa kutoka kwa watu kwamba, Diamond amekuwa akisambaza maneno mitaani kuwa haogopi vitisho vya mwanamke huyo kufuatia hatua yake ya kumrudia binti yake.
    ILIKUWAJE KWANI?
    Hivi karibuni, mama Wema alizungumza na gazeti tumbo moja la hili, Ijumaa Wikienda linalotolewa na Kampuni ya Global Publishers Ltd kila siku ya Jumatatu na kusema kitendo cha Diamond kumrudia bintiye hakubaliani nacho.
    Aliongeza kuwa, kufuatia hatua hiyo iko siku ataingia mtaani kumsaka Diamond na popote pale atakapomnasa, atamkata na panga.
    Mama Wema, Mariam Sepetu anayewasaka wapenzi hao.
    TURUDI KWA CHANZO
    “Jamani si mnakumbuka juzikati mama Wema alisema atamsaka Diamond? Sasa amesikia Diamond anatangaza mitaani kwamba, hatishiki na tamko la mama mkwe wake huyo na watakapokutana watajua nani zaidi.
    “Hivi ninavyosema, mama Wema ameingia mtaani kuwasaka. Lengo lake awakute wote wawili ili awaanzishie timbwili la kufa mtu.
    “Tangu Ijumaa iliyopita, kila siku anatoka kwenda mitaani kuwasaka, naamini siku akiwakuta pamoja kweli itakuwa vita kubwa,” kilisema chanzo chetu.
    Gari la Wema na la Diamond yakiwa yameegeshwa nyumbani kwa Wema.
    KWA NINI ASIENDE NYUMBANI?
    Chanzo kilipoulizwa kama kweli mama Wema amepania kuwanasa wawili hao, kwa nini asiwafuate nyumbani kwa binti yake, Kijitonyama, Dar ambako wanapika na kupakua, kilijibu:
    “Ameweka mtego wake pale, bahati mbaya sana Diamond naye anaishi kwa machale. Kuna siku anakwenda kulala kuna siku haendi. Huenda na yeye (Diamond) ameweka watu wake ndani kwa Wema wa kumpelelezea kama mama Wema atakwenda au ana dalili za kwenda.”
    Chanzo kikaendelea: “Siku hizi Diamond anaweza kwenda kwa Wema, akaacha gari lake na kutoka na la Wema na kurudi kwake usiku sana.”
    Paparazi wa GPL akiwa nyumbani kwa Diamond.
    AMANI LAWASAKA WAHUSIKA
    Baada ya kuzinyaka nyeti hizo, Amani liliamua kuutafuta ukweli ambapo Jumanne iliyopita lilimsaka mama Wema kwa njia ya simu lakini iliita bila kupokelewa.
    Amani lilitumia simu zake mbili kumpigia mwanamke huyo.
    Baada ya dakika tano, mama huyo mwenye ‘machungu’ na mwanaume yeyote anayemchezea bintiye alituma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) akisema: Nipo msibani tuma sms. Pia akatuma sms kwenye simu ya pili akisema: Nipo msibani, ulikuwa unasemaje?
    Amani lilimtumia madai yote kuhusu yeye kuanza kuwatafuta Wema na Diamond, pia likamjulisha kwamba kama anawatafuta kweli, muda huo, wawili hao walikuwa wapo chumbani kwa Wema hawajaamka.
    Hata hivyo, mama Wema hakujibu meseji yoyote kati ya hizo mbili hali iliyotafsiriwa na Amani kuwa, uchungu wa msiba ulimuondolea uwezo wa mawasiliano.
    Paparazi wa GPL akiongea na mlinzi wa Wema nyumbani kwake.
    NYUMBANI KWA DIAMOND
    Mapaparazi wetu walitia timu nyumbani kwa Diamond, Sinza-Mori na kukutana na mtu mmoja aliyedai ni mjomba wa staa huyo ambaye alidai Diamond Platnumz alitoka asubuhi na mama yake, Sanura Kassim kwenda Tegeta, Dar.
    NYUMBANI KWA WEMA
    Baada ya kutoka nyumbani kwa Diamond huku wakiamini Mbongo Fleva huyo kaenda Tegeta kama alivyosema mjomba mtu, mapaparazi walikwenda nyumbani kwa Wema.
    Baada ya kugonga geti kwa dakika moja, alitokea mlinzi na mambo yalikuwa kama ifuatavyo;
    Paparazi: Mambo?
    Wema.
    Mlinzi: Poa, karibu.
    Paparazi: Asante, nina shida na Wema, sijui nimemkuta?
    Mlinzi: Wamelala, hawawezi kuamka muda huu.
    Paparazi: Wamelala? Nani na nani?
    Mlinzi: Madam (Wema) na Diamond.
    Diamond.
    Paparazi: Ina maana Diamond yumo ndani?
    Mlinzi: Si nimekwambia wamelala?
    Paparazi wetu alifanikiwa kupenyeza macho kwenye nafasi ya uzio na kuyaona magari ya wote wawili, la Diamond aina ya Toyota Land Cruiser V8 na la Wema, Toyota Lexus Harrier.
    Older Posts
    © Copyright UTAMUCLASIC | Designed By Code Nirvana
    Back To Top