Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ambaye huwa haishiwi habari, ameibuka na jipya akidai kuwa akifa leo au kesho basi aagwe Uwanja wa Taifa jijini Dar, Ijumaa Wikienda limemtegea sikio.
Miss
Tanzania huyo wa 2006/07 ambaye anakimbiza kwenye sinema za Kibongo
alifunguka hayo wikiendi iliyopita wakati akiwa safarini kuelekea jijini
Arusha ambapo msanii anayemilikiwa na kampuni ya Wema ya Endless Fame
Production aliyetajwa kwa jina moja la Mirrow alikwenda kuangusha shoo
pande hizo.
Wema
aliyasema hayo alipokuwa akichangia mada ya utabiri wa mtoto wa
aliyekuwa mtabiri bingwa, marehemu Sheikh Yahya Hussein, Maalim Hassan
Hussein aliyetabiri kwamba wasanii wengi wenye majina makubwa watakufa
mwaka 2014.
Mwanadada
huyo alisema mastaa wengi wameaga dunia na kuagwa kwenye Viwanja vya
Leaders, Kinondoni lakini yeye itakuwa Uwanja wa Taifa.
Alitolea
mifano ya waliokuwa mastaa kama Steven Kanumba, Albert Mangweha
‘Ngwea’, Julius Nyaisangah ‘Anko J’ na wengine kuwa waliagwa Leaders
lakini kwa namna ambavyo jina lake ni kubwa ndani na nje ya Bongo
viwanja hivyo havitatosha.
Ijumaa
Wikienda lilipododosa kwa marafiki zake wa karibu lilitonywa kwamba
tayari jambo hilo alishawaeleza na kwamba aliomba iwe hivyo.
Mbali
na wasanii, Maalim Hassan alitabiri pia kuwa mwaka huu kuna mwanasiasa
mkubwa atakufa na utakuwa msiba wa kitaifa, vifo vya wanahabari na
malumbano makubwa juu ya serikali tatu.
Wiki
iliyopita ilijaa simanzi baada ya kufariki dunia kwa watu maarufu kama
mchekeshaji wa Futuhi ya Star TV, Omary Majuto ‘Mzee Dude’, mpiga ngoma
wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Soud Mohamed ‘MCD’,
mwigizaji wa Bongo Movies, Victor Peter na mtangazaji wa East Africa
Radio, Kenneth Kidago Lyanga
CLICK THE LINK BELOW TO WATCH THE VIDEO ONLY 1.5MB== >