Habari Kali
Loading...

UPDATES ZA MATOKEO YA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

MATOKEO: 
Mabomu yatumika: Jeshi la Polisi limeamua kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi mkoani Mwanzakatika maeneo ya Pasians, Mji Mwema, Kirumba, Ibungiro na Kitangiri baada ya vurugu wakati wa kusubiri kutangazwa matokeo.
Kijiji cha Muungano Kata ya Chahwa mkoani Dodoma: CHADEMA 196, ADC 38
Mbozi; Mtaa wa Masaki: CHADEMA 99, CCM 44
Kigoma Mjini; Mtaa wa Gezaulole: CHADEMA 240, CCM 198
Ukonga; Mtaa wa Kivule Majohe: CHADEMA 231, CCM 77
Musoma Vijijini; Kijiji cha Muhoji: CHADEMA 197, CCM 464
Ubungo; Mtaa wa Msewe: CHADEMA 683, CCM 356
Kinondoni; Mwenge Nzasa: CHADEMA 344, CCM 318
Mwanga Mtaa wa Lwami: CHADEMA 55, CCM 35
Mererani: CHADEMA imeshinda mitaa 7 kati ya 8
Kitongoji cha Endulele: CHADEMA 170, CCM 130
Monduli; Kitongoji Kambi ya Mkaa: CHADEMA 27, CCM 13
Mwanga Mtaa wa Lwami: CHADEMA 55, CCM 35
Arumeru Magharibi, Kitongoji Endulele: CHADEMA 170, CCM 130
Ushirombo Mjini: CHADEMA inaongoza vitongoji 10, CCM inaongoza vitongoji 4
Moshi Manispaa, Kitongoji Longuo A: CHADEMA 206, CCM 66
Mbozi Mtaa wa Mbugani: CHADEMA 227, CCM 160
Kata ya Mji Mpya, Morogoro yenye mitaa 12, CCM imeshinda mitaa 9, CHADEMA wakishinda mtaa 1 huku mitaa miwili mpaka sasa bado vurugu zimetanda baada ya kura kudaiwa kuzidi huku watu kadhaa wakituhumiwa kupiga kura mara mbili.
Kagondo, Kata ya Muhutwe, Kagera: CHADEMA imeshinda mitaa 4 kati ya 5
Kufungwa Vituo: Katika maeneo mengi vituo vya upigaji kura tayari vimefungwa huku wananchi wakisubiri kwa hamu kujua matokeo.
Uchaguzi Migombani: Uchaguzi wa Serikali za Mitaa eneo la Migombani, Segerea jijini Dar umeingia dosari baada ya Afisa Mtendaji Kata ya Segerea kutangaza kusitisha uchaguzi huo kimyakimya bila sababu za msingi ambapo wananchi waliamua kumweka mtu kati mpaka akaruhusu uchaguzi huo kuendelea kwa maandishi. Akijitetea afisa huyo alidai kuwa ameagizwa na Mkurungenzi wa Uchaguzi wa Manispaa ya Ilala kufanya hivyo.
Mazimbu, Morogoro: Eneo la Mazimbu, Moro kimenuka mpaka wanajeshi wamelazimika kuingilia kati kutuliza ghasia wakati wa zoezi la upigaji kura.
Kawe, Dar: Uchaguzi wadaiwa kuingia dosari baada ya mgombea wa CCM kutoa amri ya vitabu kufungwa kabla ya muda ulipangwa.
Kigogo, Dar: Mgogoro umezuka katika Kituo cha uchaguzi Kigogo jijini Dar baada ya wananchi kudai kuwa baadhi ya watu wamepelekwa kama mamluki eneo hilo kwa ajili ya kugipa kura.
Sokoine-Kibaoni, Morogoro: Wananchi eneo la Sokoine-Kibaoni, Wilaya ya Mvomero, Morogoro mpaka sasa bado hawajaanza kupiga kura mbali na wengi wao kujitokeza huku wengine wakiwa wamekodi magari kutoka Bwawa la Kihonda umbali wa kilomita 20 kwenda kupiga kura lakini mpaka sasa bado hawajapiga kura.
Amana, Ilala: Baadhi ya wananchi wameamua kususia zoezi la upigaji kura katika Kituo cha Amana, Ilala jijini Dar baada ya mgombea Uenyekiti wa Mtaa wa Amama aitwaye Mathias Ijumba kuondolewa katika uchaguzi dakika za mwisho kwa kile kinachodaiwa kuwa si mkazi wa eneo hilo lakini jambo la ajabu jina like liko katika orodha ya watu waliojiandikisha kupiga kura na mgombea huyo ameruhusiwa kupiga kura yake.
Baadhi ya wananchi wa eneo hilo wamedai jamaa huyo anakubalika sana na huenda ndiyo chanzo cha jina lake kuondolewa.
Dar es Salaam: Wananchi katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam wanalalamikia utaratibu wa majina unaotumika katika zoezi la upigaji kura linaloendelea, wengi wadai kupata tabu kuona majina yao huku wengine majina yao yakiwa hayapo kabisa katika vituo.
Shariff Shamba, Ilala: Eneo la Shariff Shamba, Ilala jijini Dar uchaguzi umeahirishwa mpaka Jumapili ijayo baada ya vifaa kutopatikana ndani ya muda muafaka. Vyama vyote vinavyoshiriki vimeafikiana.
Kagunga, Kigoma Kaskazini: Uchaguzi katika Vijiji vya Zashe na Kagunga, Kata ya Kagunga, Jimbo la Kigoma Kaskazini umefutwa hadi itakapotajwa tena baada ya Mtendaji wa Kata kuwaengua ACT katika uchaguzi huo baada ya kudaiwa kuwa wagombea wawili wa vijiji hivyo kutoka ACT walitumia anuani ya shule kama anuani yao. Hata hivyo Msimamizi Mkuu amesema anafuta uchaguzi hadi watakapotangaza tena


source -GPL

USIWE WA MWISHO;TAZAMA YALE YALIYOJIRI BAADA YA NYOKA AINA YA CHATU KUKUTWA KWA MFANYABIASHARA TAJIRI ARUSHA...

 Nyoka aina ya chatu aliyetolewa nyumbani kwa mfanyabiashara maarufu jijini Arusha Joseph Magesse akivutwa na wananchi kuelekea kwenye kanisa katoliki la karsamatiki eneo la Sakina jijini Arusha ambapo aliuawa kwa kucharangwa na shoka na wananchi wenye hasina na imani hizo za kishirikina
 ​​Kijana akiwa amembeba nyoka baada ya kucharangwa kwa mapanga akitoka naye nje ya uzio wa kanisa hilo
umati wa watu waliofika kushudia tukio hilo

 Nyumba yamfanyabishara ambapo alikutwa nyoka huyo na chini ni sehemu ya magari ya mfanyabiashra huyo
Kitambaa chenye maandishi ya kiarabu alichokutwa nacho nyoka huyokikiwa mbele ya geti la nyumba ya mfanyabiashara huyo.

MAHABUSU WAVUA NGUO KUPINGA UBAGUZI ARUSHA

Mahabusu wa Gereza Kuu la Mkoa wa Arusha, kaskazini mwa Tanzania, Jumanne walisababisha vurugu katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini humo baada ya kuvua nguo na kugoma kushuka kwenye basi lililowachukua kwenda mahakamani wakipinga kitendo cha watuhumiwa wawili wa dawa za kulevya kuachiwa huru.
Watuhumiwa wanaolalamikiwa ambao mashtaka yao yalibadilishwa mara mbili ili wapewe dhamana ni Dharam Patel na Nivan Patel wanaodaiwa kukamatwa na kete 173 za heroini na misokoto 300 ya bangi, Aprili,2014.

 

Kwa mujibu wa watu waliokuwa katika eneo la mahakama hayo, mahabusu hao walikuwa wakipaza sauti kupinga madaraja(ubaguzi) miongoni mwa watuhumiwa, wenye uwezo kifedha na wasio nacho, hali ambayo imesababisha wengine kuachiwa na wengine kuendelea kusota magerezani kwa kisingizio cha “upelelezi haujakamilika”
Mahabusu hao walisikika wakipaza sauti kutoka ndani ya basi: “Wenzetu hata mwezi haujaisha wanafutiwa kesi, jamani sisi tumekosa nini? Tunataka haki itendeke kwa wote” walisema.
Kuachiwa kwa watuhumiwa wanaolalamikiwa na mahabusu wenzao kunasemekana kumetokana na hatua ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Arusha kubadilisha hati ya mashitaka na hivyo kuwawezesha kupata dhamana.
Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa ameliambia gazeti la Mwananchi kuwa ofisi yake haina taarifa za watuhumiwa hao kupewa dhamana lakini alisema kulikuwa na jaribio la kufanya hivyo.
Bwana Nzowa amesema baada ya kubainika njama hizo, ofisi yake ilipinga, akisema kuwa kosa la watuhumiwa lilikuwa wazi na hivyo kuonyesha hali ya kutoamini kuwa watuhumiwa wanaweza kupata dhamana kwa kosa hilo!
Hata hivyo Ofisi ya Mwendesha Mashitaka, DPP haijaweza kulitolea maelezo suala la mahabusu hao kulalamikia mahabusu wenzao kupendelewa katika utoaji wa haki kwa makosa wanayotuhumiwa
Older Posts
© Copyright UTAMUCLASIC | Designed By Code Nirvana
Back To Top