Stori: Dustan Shekidele, Morogoro
KWELI ni watoto! Wanafunzi wawili, wa kike ana miaka 14 (darasa la saba), wa kiume miaka 15 (kidato cha kwanza) mjini hapa wanadaiwa kukutwa ndani ya gesti moja ikisemekana walikuwa na lengo la kuivunjilia mbali amri ya sita ya Mungu.
Tukio hilo lililojaza umati lilijiri hivi karibuni katika gesti hiyo
ambayo inadaiwa haina usajili halali iliyopo jirani na soko. Habari
zinasema kuwa, siku hiyo denti wa kike alitumwa sokoni na mama yake
kununua mahitaji mbalimbali ya chakula lakini alichelewa kurudi.KWELI ni watoto! Wanafunzi wawili, wa kike ana miaka 14 (darasa la saba), wa kiume miaka 15 (kidato cha kwanza) mjini hapa wanadaiwa kukutwa ndani ya gesti moja ikisemekana walikuwa na lengo la kuivunjilia mbali amri ya sita ya Mungu.
Ikazidi kudaiwa kuwa mama yake alimfuatilia huku akiwauliza watu, ndipo mbeya mmoja akamtonya kuwa amemwona binti yake akiingia gesti hiyo na kivulana! Mama wa watu, akiwa na mshangao, naye alizama ndani na kuwakuta chumba namba 5. Kikanuka!
Risasi Jumamosi lilifanikiwa kutinga eneo la tukio wakati wa sekeseke hilo na kuzungumza na mashuhuda wawili, Asha Chande na Tausi Omary.Walipohojiwa na mwandishi wetu walisema waliwaona wawili hao wakizama ndani ya gesti hiyo na walishangaa kwa nini walikubaliwa kwa vile wote ni watoto.
”Baada ya muda mama mmoja mtu mzima alifika hapa akiwa amefura kwa hasira, akadai binti yake aliyemtuma sokoni ameingia gesti, mara na yeye akaingia ndani, alimkuta yupo na mvulana huyo huku mfuko aliotumwa nao sokoni binti wa kike ukiwa chini ya kitanda.
“Aliwafurumusha, kivulana kimekimbia zake na huyu binti ndiyo kama hivi. Mbaya zaidi hapa ni sokoni, watu wameacha biashara na kujaa,” alisema Tausi.
Wakati sakata hilo likiendelea, baadhi ya watu walitaka kumwangushia kipondo denti huyo wa kike kwa kitendo chake cha kuacha alichotumwa na kuzamia kwenye mapenzi akiwa bado mwanafunzi.
Baadaye polisi wa pikipiki walifika na kumchukua denti huyo kwa lengo la kumuokoa na kipigo na kwenda naye Kituo Kikuu cha Polisi Morogoro ambapo ilidaiwa kuwa polisi walishauri wazazi wa watoto hao wakayamalize nyumbani.
Juhudi za mwanahabari wetu kutaka kuzungumza na mlinzi wa gesti hiyo ziligonga mwamba baada ya muda mwingi kufunga geti kubwa
GPL