Kama ni Matangazo, anzeni kulipia kodi. |
Ukiachana na hao wanaojiamini kwa kuvaa vinguo hivyo visivyowasitiri wapo wale ambao wao picha zao za vinguo hivyo vya uchi wamezihamishia katika mitandao ya kijamii kama vile Facebook ama Instagram na mingine mingi.
Sina namna ya kufanya maana hata sheria zetu (Tanzania) hazijaweza kuwabana ipasavyo kulingana na maadili ya Kitanzania ama Kiafrika kama ambavyo baadhi ya nchi zinafanya ama zimeanza kufanya kwa wale wanaovaa vinguo visivyositiri mwili, ambapo kwa ukanda wetu wa Afrika Mashariki nchi ya Uganda imetunga sheria ya kuwabana watu wanaovaa vinguo vya visivyositiri mwili hadharani hivyo wewe mwenye hiyo tabia unapaswa kusoma nyakati ukienda katika nchi kama hizo na kuna nchi nyingine wenye tabia kama hiyo hupigwa mawe hadharani.Chunga sana.
Vazi zuri kweli ila Mpasuo sasa hadi jikoni...majanga. |
Lengo kuu la kuandika haya ni kuwauliza akina dada, Nini lengo lao la kuvaa vinguo ambavyo havisiri mwili tena bila kuzingatia mazingira? Nguo ya chumbani na mmeo ama mpenzi wako wewe unaenda nayo sokoni, kweli ianwezekana? Nguo ya beach ama club wee unaenda nayo kwa shangazi ukiwa na mchumba wako kusalimia, je ni sahihi? Wakati mnatafakari maswali hayo tuwekeni wazi kama kuvaa nguo zisizositiri mwili ni matangazo ili niishauri Serikali ianze kuwatoza kodi ili uchumi wa Taifa ukue maana Serikali imeshindwa kuja na sheria ya kuwabana nyie wenye hiyo tabia.