Kati ya vitu ambavyo kwa msanii wa hapa bongo anavyojali most,miongoni mwao ni ku-maintain status yao ya u-superstar,na moja kati ya vitu anavyotakiwa kufanya mtu kama star ni kufanya vitu tofauti kabisa na mtu wa kawaida . Kwa bongo muziki umekua ukianza kulipa na pale msanii anapopata pesa hivi ndio vitu ambayo msanii wa kibongo hupata stress from:-
usafiri ,Wasanii wa bongo huumiza vichwa wanunue gari gani ili wawe kama msanii fulani au waongeze status yao. Kwa wale wasanii wadogo stress zikizidi baadhi Yao hudiriki hata kukodisha magari ya Watu na kulipa kila mwisho wa mwezi,ili tu wasionekane wakipanda daladala,tu naweza kukubaliana kuwa si kila msanii hapa bongo anauwezo wakumiliki gari kutokana tu na mauzo ya Kazi zake,cause hata underground aliyetoka na ku-hit na nyimbo moja redioni utakuta naye anahangaika na Mishe za kutaka ku-maintain status.
Mavazi , Usishangae kuona hata Nguo Watu wanagongea katika harakati tu za kuonekana unique,cause am sure si kila celeb hapa town anauwezo waku-change dress code kila siku,and Kati ya vitu ambavyo vinaongeza stress zaidi ni ujio wa instagram,social network ambayo kila celeb huwa anajitahidi ku-update Picha Yake bila ya kuonekana Kama Amerudia Nguo,cause fans lazima waliongelee Hilo, hivyo kutengeneza story mpya ya town ambayo is nzuri kWa mtu maarufu.
Nyumba, Siku za karibuni tumeona wasanii kibao wakionesha nyumba zao walizojenga na hili swala linatokana na stress wanazozipata pale wanapoona wasanii wengine wanajenga nyumba na wengine sio moja tu bali zaidi ya moja. Kwa siku za kaaribuni wasanii wengi wameonesha nyumba zao walizojenga kwa mfano linah , young D , Barnaba na Diamond. Muziki kwa sasa unalipa na hii stress ya nyumba itazidi kuongeneza kadiri siku zinavyoendelea.
Miili Mizuri , Hiki ni kitu kikubwa na kigumu kwa wasanii wengi. Msanii ni kioo na hamna msanii anayependa kuonekana akiwa na umbo baya kwahiyo wengi siku hizi hutumia muda wao kwenda gym kuweka miili yao sawa huku wengine wakiwa na personal trainers kabisa.
DISCLAIMER
Mtandao huu wa UTAMU CLASIC Unapenda Kuainisha kwamba haujashiriki kwa Namna yeyote katika Upigaji wa Picha hizi na Hautahusika kwa Namna Yeyote Ile Juu ya Malalamiko ya Aina yoyote Ile kuhusu Uchapishaji wa Habari Hii. Ingawa Tunapaenda kutoa Fursa kwa Yeyote Ambaye atakuwa amekerwa na Habari hii kutuandikia Malalamiko yake kupitia Barua pepe utamuclasic@gmail.com Nasi tutachukua Hatua stahili. Ahsante