Polisi mkoani Klimanjaro inamshikilia mzee Mungai Molel(75) kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka 11 wa shule ya msingi Okaseni na kumjeruhi vibaya sehemu za siri.
Kamanda wa Polisi mkoani humo Geofrey Kamwela, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba lilitokea Novemba 12 mwaka huu saa 12:00 jioni kijiji cha Kitandu kata ya Uru Kusini.
Kamwela alisema mtuhumiwa huyo alimwita mtoto huyo nyumbani kwake na kumfanyia kitendo hicho cha kikatili.
“Alimwita nyumbani kwake na kumbaka kwa nguvu na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri na kusababisha mtoto huyo kulazwa katika Hospitali ya KCMC” alisema Kamwela.
Kamanda Kamwela alisema mtoto huyo yupo katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa matibabu kutokana na kuharibika vibaya sehemu za siri .
Alisema mzee huyo alimbaka kwa nguvu mtoto huyo hali iliyomsababisha mtoto kupiga makelele na kuokolewa na majirani wa mzee huyo na kutoa taarifa polisi kutokana na kwamba walimkuta mtoto huyo akivuja damu nyingi.
Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi na kwamba atafikishwa mahamani upelelezi utakapo kamilika.
Aidha Kamanda Kamwela aliwataka wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini katika kufichua matukio mbalimbali ya kihalifu ili kuweza kunusuru maisha ya wananchi na mali zao, huku akiahidi jeshi kuendeleza ushirikiano huo