Na Shakoor Jongo
MCHEPUKO? STAA wa kitambo kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, Stanley Msungu amenaswa laivu akiwa kwenye pozi tata na mke wa mtu aliyetambulika kwa jina moja la Bonita.
Tukio hilo lilijiri nje ya Mgahawa wa Great Wall uliopo Masaki jijini
Dar, usiku wa saa saba ambapo kulikuwa na tafrija ya chakula cha usiku
iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve
Nyerere’.MCHEPUKO? STAA wa kitambo kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, Stanley Msungu amenaswa laivu akiwa kwenye pozi tata na mke wa mtu aliyetambulika kwa jina moja la Bonita.
“Dah! Kuna watu wana uhuru kweli na ndoa zao, yaani Bonita amefunga ndoa juzijuzi tu, mumewe amelala nyumbani yeye anahangaika huku na Msungu.
“Kama huamini nenda kwenye gari ukajionee wanachofanya Msungu na Bonita au hadi tufanye sisi ndiyo mnatupiga picha?” alihoji mmoja wa waigizaji walioalikwa kwenye hafla hiyo ambaye jina tunalihifadhi akimsisitiza mwanahabari wetu kwenda kunasa tukio hilo.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Risasi Jumamosi kama kawaida yake lilinyata hadi lilipokuwa gari la Msungu kisha kunasa tukio hilo ambapo Bonita alikuwa akijificha asionekane vizuri huku Msungu akiwa katika hali ya kutaharuki.
“Kaka mke wa mtu huyu, utaniharibia mimi na yeye kwa mumewe, achana na hayo mambo kaka njoo tuzungumze,” alisema Msungu akijitetea huku Bonita akiomba kamera ya paparazi wetu iishe chaji ili zoezi la kupiga picha lisiendelee kabla ya kuondoka eneo hilo kwa spidi na kutaka kumgonga mwandishi