Ripota
wa nguvu Simon Simalenga Dodoma amekutana na Wanachuo kwenye chuo kikuu
cha Dodoma (UDOM) ambapo kwenye bunge la bajeti linaloendelea May 19
2014 Wabunge walipitisha bajeti ya wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi
ambayo ni Bilioni 799.2
Ndani ya saa
24 toka kupitishwa kwa bajeti hiyo taarifa zinapatikana kwamba kuna
uwezekano wa kutokea maandamano ya Wanachuo wa chuo kikuu cha Dodoma
(UDOM) kuelekea bungeni kama hawatopata fedha zao za kujikimu ambazo
wamecheleweshewa kwenye collage yao ya Humanities.
Wanasema
‘hatujazungumza hivi sababu tumepanic, kikawaida chuoni tunatakiwa
kusaini boom kila baada ya siku 56 ambazo ziliisha 26 April 2014 na
mpaka hatujapata taarifa yoyote toka wakati huo kwamba kuna shida gani
imetokea’
Mwajuma Ally
ambae ni Mwanachuo wa UDOM pia amesema ‘niko mwaka wa pili, tunashindwa
kuelewa kwa nini hili tatizo limetokea mpaka sasa hivi inaonekana sisi
tunadharaulika manake hii ni mara ya pili inatokea humanities lakini
vyuo vingine wamepewa mikopo’
Wengine
wanasema ‘Wanaume wenyewe sisi wapiganaji mpaka sasa tunaumia… watoto
wa kike je?’ Mwananchuo mwingine aitwae Upendo amesema ‘hii kashfa ya
watoto wa kike kujiuza kwa Wabunge ni ya kweli kwa sababu boom
likichelewa ni bora nikakae maeneo ya bungeni kwa sababu nikimuelezea
Mbunge nina shida nitalala nae atanipa hela’
‘Ndio maana
Wasichana wengi tunapenda kujiuza, sio kwamba tunapenda kufanya makusudi
ila ni kwa sababu tunacheleweshewa hela na maeneo ya bungeni ndio
tunapendelea kwenda kwa sababu tunajua kule ndio kuna mpunga mwingi
kuliko sehemu nyingine’
Kwenye ofisi
za utawala za chuo hicho Profesa Mbunda akatoa ufafanuzi kwa kusema
‘kifupi ni kwamba management ya chuo kikuu inafatilia hilo swala, afisa
wake wa juu kabisa wa mambo ya pesa yuko Dar es salaam na ameahidiwa
katika siku tatu hili swala litakua limetatuliwa kwa hiyo tunaomba
Wanachuo wetu wavumilie kwa siku tatu’