alipotangaza kwamba deni la taifa linazidi kukua, lakini bado Serikali itaendelea kukopa fedha kutoka kwa wahisani ili kusaidi katika bajeti ya serikali ya mwaka 2014/2015,Waziri huyo anakabiriwa na tuhuma nzito ya Ufisadi mkubwa na wakutisha.

Waziri
Mkuya anatuhumiwa kwa kuandaa safari ya watu zaidi 30 kwa kutumia kodi
za watanania, kwenda nchini Sweden kujifunza masauala mbalimbali ya
bajeti na ukusanyaji wa kodi. Safari hiyo itawajumuisha wajumbe wote wa
kamati ya Bajeti ya Bunge pamoja na maofisa wa Wizara ya Fedha.
Chanzo cha Habarimpya.com cha kuaminika kutoka katika Wizara hiyo kinadai kwamba, safari hiyo inatokana na kikao cha ndani kilichofanyika hivi karibuni Wizarani hapo. kilichokuwa na lengo la kuandaa mazingira ya Bajeti ya Waziri huyo kupitishwa bila kupingwa katika Bunge la bajeti.
Chanzo hicho kilifafanua kwamba baada
ya majadiliano ya kina kuhusu mbinu mbalimbali, zitakazo tumiwa na
Waziri huyo ili bajeti yake iweze kupitishwa ndipo wazo la safari hiyo
ilipoibuliwa.
Safari hiyo ya siku 11 inaratibiwa naKatibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Alphonce
Mayala,aliyeandika barua ya kuijulisha serikali ya Sweden kupitia
Ubalozi wake kuhusu nia na sababu ya safari hiyo.
Katika barua hiyo ambayo iliandikwa jana na Habarimpya.com kudaka
nakala yake iliwataja wajumbe 10 wa Kamati ya Bunge la Bajeti kuwa ni
pamoja na Waziri wa Fedha Saada Mkuya,Amina Abdulla Amour,Christine
Mughway Lissu,Kidawa Hamid Saleh,Dk Bulugu Fetus Limbu na Saleh Pamba, Peter Joseph Serukamba,Michael Chikokoto,Elisa Daniel Florian Mbise,na Mohamed Hamad Rashid.
Wengine ni pamoja na Mpina Joelson
Mpina kutokana tume ya viwanda na biashara,Khatibu Said Haji,Ahmed Juma
Ngwali,Vicky Pascal Kamata,Joyce John Mukya,David Zakaria Kafulila, wote
kutoka kamati ya Uchumi,Viwanda na Biashara.
Wajumbe kutoka Wizara ya Fedha ni
pamoja na,Adolf Faustine Mkenda,John Mihayo Cheyo,Pius martin
Mponzi,Charles Ambele Mwamwaja,Susana Benard Mkapa,pamoja na Thimas
Mabeba Nyamara. Safari hiyo ambayo inatarajia kufanyika kati ya tarehe 02 - 12 Februari, 2014 imebatizwa jina la 'Study Tour' kwa ajili ya kujenga uwezo kwenye mambo ya bajeti na ukusanyaji wa mapato
credit: Habari mpya.com
CLICK THE LINK BELOW TO WATCH THE VIDEO ONLY 1.5MB== >