Habari Kali
Loading...

Undani wa ajali ya gari iliyoua Askari Polisi watano papo hapo mkoani Dodoma usiku wa kuamkia leo ..

CLICK THE LINK BELOW TO ENTER IN THE CHANCE OF WINNING== >

 Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma
 ****
Askari polisi watano mkoani Dodoma wamefariki dunia papohapo katika ajali ya gari iliyotokea 31/01/2014 majira ya 23.45 hrs katika barabara kuu ya Dodoma – Morogoro eneo la Mtumba Center, Kata ya Mtumba Tarafa ya Kikombo Manispaa ya Dodoma, ambapo gari namba T.770 ABT Toyota Corolla lililokuwa likiendeshwa na Askari namba H. 3783 PC DEOGRATIUS wa Polisi Wilaya ya Kongwa likitokea Dodoma mjini likielekea Wilayani Kongwa liligongana uso kwa uso na gari namba T.997AVW Scania Bus mali ya Kampuni ya Mohamed Trans lililokuwa likiendeshwa na JUMA s/o MOHAMED, miaka 38, Mkazi wa Mwanza, likitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma na kusababisha vifo kwa askari watano papohapo. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME amewataja Askari hao waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni:-
 
1.          D.9084 D/CPL. ADOLF S/O MESHACK SILLA mwenye miaka 51, Mgogo.
2.          F.6459 D/C. EVARIST s/o MOSES BUKOMBE mwenye miaka 34, Muha.
3.          H.3783 PC. DEOGRATIUS s/o PATRICK MAHINYILA mwenyw miaka 29, Mgogo.
4.          WP.10337 PC. JACKLINE d/o AUGUSTINE TESHA mwenye miaka 22, Mchaga.
5.          WP.10382 PC. JEMA d/o JIMMY LUVINGA mwenye miaka 20, Mhehe. 
Wote ni askari Polisi Wilaya ya Kongwa na hakuna abiria aliyeumia katika basi.

Kamanda MISIME amesema chanzo cha ajali hiyo kulingana na uchunguzi wa awali ni mwendo kasi kutokana na uharibifu uliotokea kwa gari dogo walilokuwa wamepanda askari na jinsi lilivyoburuzwa na basi kwa umbali wa mita 56 kisha kwenda kusimama umbali wa mita 97, kwa hali hiyo umbali kutoka eneo walipogongana hadi basi liliipoenda kusimama ni mita 152. Dereva wa Bus alitoroka mara baada ya ajali hiyo kutokea, juhudi za kumtafuta zinaendelea. Miili ya maerehemu imehifadhiwa chumba cha maiti Hospitali ya mkoa Dodoma.

Aidha Kamanda MISIME ametoa  wito kwa madereva kila mara wawe na udereva wa tahadhari na kuzingatia sheria za usalama barabarani.

CLICK THE LINK BELOW TO WATCH THE VIDEO ONLY 1.5MB== >
After the long storry that has been taking over the internet about prizes and gifts here are some of the prizes that our customers are going to win as you see the bellow is the heading which show you that if you press down their is the link that if u press your going directly into a chance that will enable you to enter into the competition so dont hestitate you just click below what you need is to click fast so as the chance cant bypass you since it doesnt come twice it only comes in a single tyme specified for your fortune/lucky: CLICK THE LINK BELOW TO ENTER IN THE CHANCE OF WINNING== >
Newer Posts Older Posts
© Copyright UTAMUCLASIC | Designed By Code Nirvana
Back To Top