AMA kweli dunia imefika ukingoni! Ile Oparesheni Fichua Maovu (OFM),
bado ipo kazini ikishirikiana na polisi ambapo safari hii imeibuka na
kigongo cha aina yake baada ya kumnasa ‘mwanaume tata’ akijihusisha na
ukahaba, Risasi Mchanganyiko lina mzigo kamili.
Ikiwa
kwenye fumuafumua ya magenge ya ngono maeneo ya Kahumba mjini Morogoro
hivi karibuni, OFM kwa mwaliko wa jeshi la polisi, ilipigwa na butwaa
baada ya kukutana uso kwa uso na mwanaume huyo aliyekuwa amejumuika
katikati ya kundi la madadapoa naye akifanya kama wao.
Mbali
na jamaa huyo ambaye jina lake halikupatikana, baadaye ilibainika kuwa
kulikuwa na wenzake wawili ambao ilikuwa vigumu kuwatambua kufuatia
kujiremba kupita hata wanawake wenyewe.
Kuna
madai kwamba kijana huyo aliyekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 20
- 24 ni mtoto wa kigogo serikalini na amekuwa akijichanganya na
madadapoa hao kwa muda mrefu.
Mara baada ya kunaswa, kijana huyo aliangua kilio huku akidai kuumbuka kwani familia yake wakiiona picha yake hawatamwelewa.
“Naombeni
tumalizane hapahapa kwani nyumbani hawafahamu kuwa nipo hapa muda huu.
Hii ni kesi kubwa kwangu nisaidieni,” alisikika kijana huyo.
Hata
hivyo, pamoja na kilio hicho, polisi hawakumwelewa, alibebwa juujuu na
kuingizwa katika karandinga kisha kutupwa nyuma ya nondo za mahabusu
kusubiri sheria kuchukua mkondo wake.
Wakazi
wa maeneo hayo walikuwa wakilalamika mara kwa mara kutokana na
kurundikana kwa makahaba mahali hapo na kusababisha uchafuzi wa
mazingira kwa kutupa ovyo mipira ya kiume (kondom).
Katika msako huo, wanaume hao watatu walijumuishwa na wanawake 20 waliokamatwa wakijihusisha na biashara haramu ya kuuza miili.
-GPL
CLICK THE LINK BELOW TO WATCH THE VIDEO ONLY 1.5MB== >