SIKU chache
baada ya Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) kuzuia filamu ya mkongwe katika
sinema za Kibongo, Mahsein Awadh Said ‘Dk. Cheni’ ijulikanayo kwa jina
la Nimekubali isiingie sokoni kwa madai kuwa imekiuka maadili ya
Kitanzania, msanii huyo ameibuka na kueleza kinagaubaga, Risasi Jumamosi limenasa sauti yake.
Akizungumza
na mwandishi wetu Jumatano ya wiki hii maeneo ya Mlimani City jijini
Dar, msanii huyo alisema amesikitishwa na maamuzi ya bodi hiyo huku
akidai kuwa lengo la filamu hiyo ni kukemea tabia za kishoga
zinazoendelea kuibuka kwa vijana ikiwa ni pamoja na kupinga uhalali wa
ndoa za jinsia moja.
Katika
maelezo hayo, DK. Cheni ambaye huzitendea haki filamu zake kwa kuvaa
uhusika halisi, alisema moja ya kigezo ambacho bodi hiyo imekitumia
kuzuia filamu hiyo ni pamoja na muonekano wa bango la filamu hiyo ambalo
linamuonesha msanii huyo akiwa amevaa vazi la shera huku akiwa
amejiremba kwa madai kuwa ni kuchochea ushoga jambo ambalo msanii huyo
amelipinga vibaya.
“Eti
ushoga wangu uko kwenye kujiremba sana, hakika wamenionea sana, lengo
letu ni kuonya na kukemea vikali vitendo vya ushoga na ndoa za jinsia
moja, huwezi kuelimisha bila kuonesha madhara yake kwa vitendo kama
ilivyo ndani ya filamu hiyo.
“Lakini,
ndani ya filamu hiyo, kuna kipande ambacho kinaonesha kiongozi wa
serikali akikemea kitendo hicho, sasa hapo ushoga wangu uko wapi?
Kuvalia shera kwenye kava? Siyo sahihi,” alisema Dk. Cheni.
Mbali na kava hilo, msanii huyo alidai haoni kosa lolote katika filamu hiyo hivyo ataendelea kupigania haki yake na kwamba hayuko tayari kuonewa.
Mbali na kava hilo, msanii huyo alidai haoni kosa lolote katika filamu hiyo hivyo ataendelea kupigania haki yake na kwamba hayuko tayari kuonewa.
Jitihada
za kumpa mkurugenzi wa bodi ya filamu, Joyce Fissoo ili kuelezea juu
ya sekeseke hilo, ziligonga mwamba hadi gazeti hili linaingia mtamboni
lakini imedaiwa kuwa bodi hiyo itasimamia msimamo wake.