Na Chande Abdallah
ILE Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ chini ya Global Publishers ipo kazini! Safari hii imekutana na tukio la aina yake baada ya kumnasa kikongwe mmoja anayedaiwa kumiliki idadi kubwa ya madanguro katika uwanja wake na kuwapangisha makahaba katika eneo maarufu kwa jina la Kijiji cha Makahaba.
Awali kachero wa OFM alipokea ujumbe mfupi ulioelezea ufuska unaofanywa
na mabinti ambao hupewa eneo na kujenga vibanda kisha kujiuza kwa bei
chee katika kijiji hicho maeneo ya Kigamboni jijini Dar.
Mzee Matutu ambaye ni mmiliki wa eneo linalofanyiwa ufuska.
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kwamba, eneo hilo linalofanyiwa ufuska huo
linamilikiwa na kikongwe aliyejitambulisha kwa jina la mzee Matutu akidaiwa
kuendesha maisha kwa biashara hiyo ya madanguro.
Baada ya kujiridhisha na uchunguzi kuwa ni kweli jambo hilo linafanyika eneo
Baada ya kujiridhisha na uchunguzi kuwa ni kweli jambo hilo linafanyika eneo
hilo, OFM ililivamia ikiwa na mjumbe wa mtaa huo aliyefahamika kwa jina la
Abbas na kujionea madanguro yaliyojengwa kwa mstari ambapo milango yake
iliachwa wazi huku ndani wakionekana mabinti wakiwa wamejilaza kihasarahasara
wakiwatega wateja wanaopita katika mtaa huo.
Madanguro hayo ambayo kwa hesabu ni takriban kumi na nane, yamejengwa
Madanguro hayo ambayo kwa hesabu ni takriban kumi na nane, yamejengwa
kwa aina yake ambapo mengi kati ya hayo yana ukubwa wa kutosha kuingia kitanda
kidogo pekee.
Baada ya kujionea hayo, kikosi kazi sambamba na mjumbe huyo kilimtafuta
Baada ya kujionea hayo, kikosi kazi sambamba na mjumbe huyo kilimtafuta
mzee Matutu na kufanikiwa kuzungumza naye kuhusu madanguro hayo na
namna anavyoyaendesha ambapo alikiri kuwa yeye ni mmiliki wa eneo hilo na
huwa anapokea shilingi 30,000 kwa mwezi kwa kila mwanamke na fedha hiyo
ndiyo inayomsaidia kuendesha maisha.
“Sina kazi nyingine ya kuniingizia kipato zaidi ya hii ya wasichana licha ya
“Sina kazi nyingine ya kuniingizia kipato zaidi ya hii ya wasichana licha ya
kwamba sijawaruhusu wafanye biashara hiyo. Fedha hiyo ndiyo inanisaidia
kwa mahitaji yangu,” alisema kwa tabu mzee Matutu huku akimtaja msimamizi
wa madanguro hayo kuwa ni mpwa wake.
Kwa upande wake mjumbe wa mtaa huo, Kassim alisema kuwa serikali ya
Kwa upande wake mjumbe wa mtaa huo, Kassim alisema kuwa serikali ya
mtaa imejitahidi kwa kadiri ilivyoweza kuwaondoa mabinti hao lakini
wamekuwa wakirudi kila mara.
Alipoulizwa hatua waliyoichukua kwa mmiliki wa madanguro hayo ambaye
ni mzee Matutu, kiongozi huyo alibakia kusikitika asijue hatua gani ya
kumchukulia mzee huyo ambaye hata wakimpeleka kwenye vyombo
vya sheria anahisi itakuwa ni uonevu kwa kuwa hana msaada mwingine wa
kifedha zaidi ya fedha kutoka kwa mabinti hao.
CREDIT-GLOBALPUBLISHERS