Aliyejipachika
kuwa dada wa hiyari wa Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
ambaye ni zao la Shindano la Kimwana Manywele, Halima Haruna ‘Kimwana’
amefungukia ishu ya mastaa kibao kujitongozesha wenyewe kwa jamaa huyo
Halima Kimwana alielezea sakata hilo
wikiendi iliyopita baada ya kuulizwa undani wa skendo inayomkabili ya
kumkuwadia au kumtongozea Diamond kwa mastaa na kuwabadilisha kama nguo.
Kwa mujibu wa Halima Kimwana, huwa Diamond hajisumbui kumtongoza mwanamke zaidi ya hao mastaa kujitongozesha wenyewe kwake.
Halima Kimwana alidai kwamba yeye kama
dada wa mwanamuziki huyo (hakutaka kufafanua dada kivipi), amefikia
hatua ya kusumbuliwa na wasichana wa kila aina hasa mastaa wakimuomba
awatongozee kwa Diamond tena kwa ahadi kemkemu.
“Kwani unafikiri Diamond anajihangaisha kuwatongoza hao mastaa? Wao
ndiyo kila kukicha wanamsumbua na kutuhangaisha sisi wakitaka
tuwatongozee kwa kaka yetu.
Tena wengine wanatoa ahadi nyingi tu
kama tukiwafanikishia,” alisema Halima Kimwana na kuongeza kuwa katika
listi hiyo ya mastaa wanaojitongozesha kwa Diamond, wapo mastaa wakubwa
ambao anawahifadhi ili asiwavunjie heshima.
CREDIT - GPL